Mbunge Peter Msigwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika hivi;-
 "Msigwa amekamatwa na Polisi huko Iringa na kushushwa kwa nguvu jukwani  ktk Mkutano halali. Msiogope baada ya giza nene asubuhi hutokea!"
Taarifa hiyo iemethibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishna wa polisi Julius Mjengi, Ambapo ameuleza mtandao huu kuwa Msigwa alikuwa na mkutano wa hadhara leo Septemba 24, katika eneo la Mlandege mkoani humo ambapo anadaiwa kutumia lugha na matamshi ya uchochezi katika hotuba yake.

Hata hivyo Kamanda Mjengi ameongeza kuwa tayari wameanza kumuhoji

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search