Mtatiro Aivaa Serikali ya JPM...Ni Baada ya Kukamatwa kwa Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360
SAA chache baada ya Mbunge wa Iringa mjni Peter Msigwa Kukamatwa na Jeshi la Polisi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro amesema kukamatwa kwa Msigwa ni mwendelezo wa Uimla na ukandamizaji unaofanywa na serikali dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani.
"Kukamatwa kwa Mhe. Peter Msigwa, mbunge wa Iringa Mjini ni mwendelezo wa Uimla na Ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya sasa dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani. Na ni njia ile ile ya sasa ya kukandamiza demokrasia nchini." amesema Mtatiri kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishna wa polisi Julius Mjengi ameueleza mtandao huu kuwa Msigwa alikuwa na mkutano wa hadhara leo Septemba 24, katika eneo la Mlandege mkoani humo ambapo anadaiwa kutumia lugha na matamshi ya uchochezi katika hotuba yake.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment