Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo Atangaza Kung'atuka Nafasi Hiyo Leo...Habari Kamali Hii Hapa na Matukio360...#share
MWENYEKITI wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi (CCM) Taifa Abdallah Bulembo amesema atamwandikia barua Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kueleza nia yake ya kutokugombea tena nafasui hiyo kwa mara nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Bulembo amebainisha kuwa alirudisha nia ya kuwania tena nafasi hiyo baada ya kushawishiwa na wazee wachama hicho akiwemo Mzee John Malecela.
"Leo nimewaiteni hapa kuwaeleza kuwav nitamkabidhi barua Katibu Mkuu wangu yakumweleza kwamba sitagombea tena, nafanya hivi ili kupumzika na kuachia kijiti hiki watu wengine wakiendeleze," amesema Bulembo.
Aidha amesema kuwa hadi sasa wanachama 49 wamekwisha chukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya kumrithi na ameeleza kwamba anauhakika miongoni mwa wagombea hao wapo wenye sifa ya kuiongoza Jumuiya hiyo.
Bulembo ameeleza kuwa katika kipindi chake akiwa kama kiongozi anajivunia kuweza kulipa asilimia 65 ya sh.bilioni 4.8 deni alilikuta ikidaiwa Jumuiya hiyo, pia wamefanikiwa kununua pikipiki mikoa yote nchini.
Ameongeza kwamba alikuta wakiwa na viwanja 16 lakini hadi anapomaliza muda wake wanavyo zaidi ya 48. Amebainisha pia alikuta wakiwa wanaingiza mapato ya sh.milioni 50 kwa mwaka lakini mwaka wa kwanza akiwa kiongozi yaliongezeka makusanyo hadi sh. milini 900.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa pili katika uongozi wake makusanyo ya mwaka yamefikia kiasi cha sh. bilioni 4.6, kadhalika ameacha wakiendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa 12.
Akizungumzia uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea ambao umefika katika hatua za Wilaya na Mikoa amesema Makatibu Wakuu wa Ngazi hizo watapimwa kwa kufanikisha chaguzi hizo na kuhakikisha unakuwa wa haki na kupatikana viongo, huku akieleza watakao shindwa kusimamia watamfukuza.
Aidha amebainisha kuwa uchaguzi ngazi ya Taifa utafanyika kuanmzia Novemba 20 hadi 23 mwaka huu ambapo atamweleza Mwenyekiti wa Chama hicho Rais John Magufuli mali na kiasi cha fedha alichoacha ndani ya Jumuiya.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment