Zari Amuonya Diamond Kuhusu Hamisa Mabetto kwa Kumtolea Povu Zito...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360#share

SAKATA la Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasibu Abdul Maarufu kama Diamond na mwanamitindo Hamisa Mobetto limechukua sura mpya baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe katika masuala yao.

Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo tena.

Wakati Diamond akiendelea na mahojiano katika kituo cha Clouds FM, Zari aliandika katika mtandao huo akisema, 
“Hahahaha unajidanganya, unasema uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno yako.”

Aliendelea kuandika: “Inawezekana mimi ni mama wa watoto wako ndio maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda ugoogle kuhusu ‘defamation of character law suit’, usinijaribu.”

Diamond alipoulizwa kuhusu kauli hizo amesema anamwelewa kwa kuwa kuna baadhi ya mambo hakumweleza na kwa mara ya kwanza huenda ameyasikia wakati huo.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search