Savio Mabingwa StarTimes RBA 2017..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
TIMU ya Mpira wa
Kikapu ya Savio imekuwa mabingwa wa Ligi
ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam kwa upande wa wanaume (Dar e Salaam Stertimes
RBA) kwa mwaka 2017 baada ya kuwachapa mabingwa watetezi JKT Mgulani kwa pointi
88 dhidi ya 81 katika fainali iliyopigwa jana kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.


Fainali hiyo ilikuwa ni ya shindano la 33 ambapo bingwa huyo
mpya alikabidhiwa zawadi ya sh. 700,000 na Medali za Dhahabu huku JKT ambaye ni
mshindi wa pili akipatiwa sh. 500,000 na
medali.
Aidha kwa upande wa kina dada bingwa amekuwa ni Timu ya
Vijana Queens. Imetwaa ubingwa huo baada ya kuichapa Timu ya Donbosco kwa
pointi 72 dhidi ya 69.
Kwa huo Vijana Queens pia wamekabidhiwa kitita cha sh.700,000
na medali za Dhahabu huku Donbosco wakikabidhiwa sh. 500,000 na medali.
Washindi wa tatu kwa pande zote wamepatiwa sh.300,000 kila
mmoja ambapo kwa wanaume ni Vijana City Bulls huku kwa wanawake ikiwa ni JKT
Stars.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi
Makamu wa Rais wa Kampuni ya StarTimes nchini Zuhura Hanif, amesema kupitia udhamini wa RBA ni mwanzo wa
kuwa karibu na jamii kwa kuwapa vijana ajira kupitia michezo.
“Huu ni mwanzo wa kuwa karibu na jamii, lakini pia kuwapa
vijana ajira pamoja na kuwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,” amesema Hanif.
No comments:
Post a Comment