Sued Kubenea Ashikiliwa Na Jeshi la Polisi...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
WAKATI serikali ikiwa imelifungia Gazeti la Mwanahalisi
ambalo linamiliwa na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea ,KATIKA hali isiyokuwa ya
kawaida, polisi wenye silaha wamezingira hospitali ya Agha Khan aliyokuwa
ameenda kupata huduma ya matibabu, Mbunge
Kubenea na kumsubiri atibiwe kisha kuondoka naye.
Taarifa zinasema polisi hao wameelekea kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam ingawa haijajulikana wanapompeleka na kwa kosa gani.
Wiki iliyopita Spika Job Ndugai aliviagiza vyombo vya dola
kuwakamata Kubenea pamoja na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe na kuwafikisha
mbele ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama.
Hii inatajwa kuwa Mbunge huyu anapitia naye katika kipindi
kigumu kwenye cha awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli tangia iangie
madarakani amekumbana na misukosuko ya Biashara zake za Magazeti kutokana
serikalii hii kuyafungia Magazeti yake yote.
Magazeti yake hayo ni Mawio,Mwanahalisi pamoja Mseto ambayo
yamefungiwa kutokana na kuandika habari zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.
No comments:
Post a Comment