Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Asikitika Kuzuliwa Jambo Mitandaoni.... Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360.. #share
RAIS Msaafu wa Awamu ya Nne amezuliwa jambo katika mitandao ya kijamii.
Katika hali ya kushangaza kumekuwa na ujumbe unaosambaa katika mtandao wa Facebook ukionyesha kunukuu maneno ya Rais Kikwete ambayo yanaonyesha kama kuipiga dongo Serikali.
Ujumbe huo unasema "Pale unapomuona mtu anajaribu kumlazimisha Mbwa asibweke wakati ni sehemu yake kubweka lazima utajiuliza huyu mtu utumia nini wakatio wakufikilia,"
"Lakini naomba mtambue kuwa unapokuwa kiongozi unapokuwa na busara na kuheshimu maoni ya watu wa pembeni yako utaqhishia kuwamaliza viongozi wenzako ukihisi ni maadaui," umesema ujumbe huo
Kufuatia ujumbe huo Rais Kikwete amatoa neno kupitia ukurasa wake wa Twitter kukanusha suala hilo akisema,
"Nasikitishwa sana na uvumi huu unaosambazwa juu yangu.Inasikitisha sana. Inasikitisha zaidi kuwa wako watu timamu wanaoamini uzushi huu," ameandika Rais Kikwete.

Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment