TECNO yafanya hafla maalumu kuwapongeza washindi wa SPARK jijini Mwanza...#share

Kampuni ya TECNO imeonesha ni kwa jinsi gani inathamini wateja wake kwa kuaandalia hafla maalumu  kuwapongeza wateja  wa simu mpya ya TECNO SPARK.

Mkuu wa mauzo kwa Upande wa TECNO mkoani Mwanza akiwa tayar kukabidhhi zawadi kwa mshindi.

TECNO inayofanya kampeni ya simu mpya iliyopatia umaarufu mkubwa nchini TECNO SPARK imewaandalia wateja wake hafla ya maalumu ya kuwashukuru  kwa kuwaunga mkono pamoja na kuwapa zawadi za  aina mbalimbali ikiwemo simu mpya  ya TECNO SPARK iliyokwenda kwa mshinid bwana Baraka Modo mkazi wa Mwanza.

Akizungumza wakati wa hafla  hiyo ,Afisa Mahusiano wa TECNO bwana , Eric Mkomoye amesema kwamba TECNO inaendeleza utaratibu wake wa kuwajali wateja wake kupitia  matukio mbalimbali yatakayokua yanaandaliwa kwa nia ya kuwapongeza wateja wa TECNO na kuwaweka karibu na kampuni hiyo kama ambavyo mteja wao katika hafla hiyo bwana  Baraka Modo alivyojishindia TECNO SPARK.
Mshindi wa SPARK Bwana, Baraka Modo akikabidhiwa zawadi yake na timu ya mauzo ya TECNO mkoani Mwanza.
Wateja wa Tecno mkoani Mwanza  walipata nafasi ya kuingia kwenye hafla hiyo maalumu iliyoitwa TECNO BLUENIGHT baada ya kununua simu ya TECNO SPARK, huku wengine wakipata tiketi kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO.

TECNO inaendelea kuwahimiza wateja wake kujumuika katika kampeni mbalimbali inazoziendesha ili  wateja waweze kufaidika zaidi.
Timu  ya TECNO ikiwa  tayari kwa hafla maalumu jijini Mwanza.

Simu iliyowezesha wateja hao kuwepo katika hafla hiyo maalumu ni TECNO SPARK simu mpya iliyojipatia umaarufu mkubwa nchini kwa umbo lake la kuvutia, ikiwa ina usalama wa alama za vidole (finger print), kioo chake ni kikubwa huku ikiwa na camera ya 13mp nyuma na 16gb za kuweka data za aina zote katika simu bila kutumia kadi kumbukumbu (Memory kadi). 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search