Wasanii Nchini Washauriwa Kufanya Kazi na Taasisi za Kifedha...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
WASANII wa tasnia mbalimbali nchini wameshauriwa kufanya kazi
kwa kuzitumia taasisi za kifedha ili waweze kupata fursa za mikopo, wafadhili
na uingiaji mikataba itakayosaidia uendeshaji wa makundi yao.
Katika picha wa katikati ni 0fisa Masoko wa Benki ya DTB, Ally Mbwana, Kushoto kwake ni ofisa mwenzie, Lisa Mugerezi Na Kulia kwake ni Mtendaji Wa Basata, Rajab Solo wakizungumza katika jukwaa la sanaa jijini Dar es Salaam Leo.
Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Afisa
Masoko wa Benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Ally Mbwana katika Jukwaa la Sanaa
lililokuwa likijadili umuhimu wa wasanii kufanya kazi na taasisi hizo.
Amesesma wasanii wamekuwa wakishindwa kupiga hatua kutokana
na kutoshrikiana na taasisi za fedha ikiwemo ufunguaji akaunti za makundi hali
inayowasabishia kukosa mikopo na wafadhili wenye nia kuyaunia makundi hayo.
Amesisitiza kuwa makampuni mengi hayawezi kusaini mikataba na
vikundi vya sanaa bili kuhakikisha kikundi kina mwongozo wa akaunti madhubuti.
Amewashauri wasanii kuchangamkia fursa za DTB kwa kufungua
Akaunti Maalum kwa ajili ya vikundi vyao kwa gharama ya Sh 100,000 huku
akibainisha akaunti itawasaidia kuhifadhi fedha zao na kulipia gharama za kodi
ya majengo.
Kwa upande wake Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa
(Basata), Rajab Solo ameipongeza benki hiyo kwa mipango madhubuti yenye lengo
la kuwakomboa wasanii.
Naye Msanii wa maigizo, Mcdonald Hule ameiomba benki hiyo
kufikiria mpango wa kuanza kutoa elimu ya mikopo itakayowasaidia kwenye ununuzi
wa vifaa vya muziki na uimarishaji makundi.
Msanii Maraiam Mponda'Mama Mipango ameishukuru benki hiyo na
kuiomba iendelee kuwasaidia kutoka mahala waliko na kutambulika kimataifa.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment