Wizara ya Afya Yapokea Msaada wa Mashine ya Kutoa Dawa ya Usingizi...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imepokea msaada
kutoka kwa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) wa mashine ya kutoa dawa ya usingizi wakati wa upasuaji yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 60.
Akipokea msaada huo leo jijini Dar es Waziri wa Wizara hiyo
Ummy Mwalimu, amesema mashine hiyo itasaidia kupunguza vifo vya watoto na akina
mama wakati wa kujifungua.
“Kwa mujibu wa takwimu ni kwamba hivi sasa wanawake 30
hufariki kila siku, inamana kuwa kwa mwezi hufariki wanawake 900,” amesema
Waziri Ummy.
Aidha Ummy amesema katika kuhakikisha wanaboresha mazingira
ya huduma za afya kwa wazazi na watoto ni kwamba serikali imejipanga kabla ya
mwezi Juni mwakani kuongeza vituo vya 170 vya kutoa huduma ya uzazi kote
nchini.
Waziri Ummy ameongeza kuwa serikali imetenga sh.bilioni 8 kwa
ajili ya kununulia vifaa pamoja na dawa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya
ili kukabiliana na vifo vya akina mama hao na watoto.
Kwa upende wake Mratibu wa Taifa wa WRATZ Rose Mlay, amesema
lengo la msaada huo ni kwa sababu wameona kuwa wanao wajibu wa kusaidia kuokoa
maisha ya wazazi na watoto wakati wa kujifungua.
“Mashine hii itatumika kunusuru maisha ya mama na mototo,
lakini na watu wengine. Hili ni jambo la kujivunia,” amesema Mlay.
Akitoa ufafanuzi wa jinsi inavyofanya kazi mashine hiyo, Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Mpoki Ulisubisya
amesema inauwezo wakutengeneza asilimia 21 ya hewa ya oksijeni kwa ajili ya
kumsaidia mgonjwe.
Aidha amesema kuwa hata umeme unapokatika ina uwezo wakutumia
hewwa ya oksijeni ya kawaida ambayo inatumiwa na watu wengine.
Dk. Ulisubisya amesema msaada huo ni hatua kubwa katika
maendeleo ya uboreshwaji wa huduma za afya nchini, lakini amesema kuwa
kinachotakiwa kwa sasa ni kuandaa wataalamu wakutumia mashine za jinsi hiyo.
Mashine ya kutoa usingizi wa kati wa huduma ya upasuaji msaada uliotolewa kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo jijini Dar es Salaam na WRATZ
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment