Burudani: Kampala City Festival yabainisha 'upevu wa Diamond Platnumz kikanda na kimataifa'.. ajizolea Mil. 700 #share

KATIKA hali iliyoonekana ni 'ukuu wa wa msanii Diamond Platnumz' kikanda na Kimataifa,.. waandaaji wa Tamasha la Uganda-Kampala City Festival Nchini Uganda lililofanyika jioni ya kuamkia jana, wamemlipa kitita kikubwa cha shs. Mil. 500 za kibongo takriban shs. 700 Milioni za kiganda, na kuzua taharuki kubwa nchini humo.
Baadhi ya wasanii wa Uganda wamelalamikia Diamond Platnumz kulipwa fedha nyingi kiasi hicho kwa kuperfom usiku mmoja katika tamasha hilo, huku msanii maarufu zaidi eneo hilo akilipwa 4 million za Uganda. 

Katika hatua iliyoonekana kuzua sintofahamu kubwa miongoni mwa wasanii wa Uganda, ni kitendo cha waandaaji hao kumpa Diamond heshima ya 'wa Kimataifa' International Artist' msanii huyo wa bongo ambaye ndie alikuwa mtumbuizaji mkuu katika Tamasha hilo. 

Kufuatia hatua hiyo, baadhi ya waganda hususan wasanii, wameungana kupinga malipo hayo makubwa kwa Diamond, ambapo wasanii wa ndani wengi wao walioperform kwenye Tamasha hilo wakiambulia milioni mbili-mbili.

Lakini katika hatua tofauti,  baadhi ya waganda wametoa mtazamo tofauti wakidai kuwa alichokifanya 'shemela' wao kwenye jukwaa kinaendana na malipo hayo.

wamesema kwa hadhi yake Diamond, ambae mzazi mwenza wa Zari the Boss Lady,.. anastahili, na wanachotakiwa kufanya wasanii wa Uganda ni 'kukaza buti' na kufanya muziki wa kimataifa ili malipo yaongezeke.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search