DC Mnyeti Awakana Lema na Nassari...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti amewajibu mapigo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki.

Amesema video zote ambazo anasambaza Nassari ni za mikutano yake akiwa Kwenye shughuli za maendeleo za Wilaya.

DC ARUMERU: "Video zote anazosambaza Nassari ni za mikutano yangu nikiwa Kwenye shughuli za maendeleo za Wilaya,upinzani huu umekosa dira"

DC MNYETI: "Nilimchangia mchango wa harusi diwani aliyehamia ccm kama ambavyo nimekuwa nikiwasaidia madiwani wengi waliopo CDM akiwemo Nassari"

DC MNYETI ARUMERU: "Nassari aweke pia video ambazo tumekaa nae akinieleza matatizo ya jimboni kwake."

DC ARUMERU: "Watumishi kumchangia harusi Diwani ndiyo rushwa wanayosema Chadema.Ila nilipoombwa kuchangia matibabu ya Lissu haikuwa rushwa"

Credit: DarMpya

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search