Dereva wa Lissu Alichanganya Jeshi la Polisi..IGP Sirro Aibuka na Hili...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema wanapata shida juu ya habari za kwamba dereva wa Lissu yuko nchini Nairobi anatibiwa kisaikolojia wakati kwenye magazeti anaonekana akiwa ameng'aa.
IGP Sirro amezungumza maneno hayo leo alipokuwa ziarani mkoani Mtwara ambapo ametuma salamu za kumtaka dereva wa Lissu  kurudi nchini kulisaidia jeshi hilo katika kukamilisha upelelezi wake juu ya tukio la shambulio kwa kiongozi huyo.

“Yule kijana kwenye picha ukimwona yuko vizuri tu, sasa wanaposema anapata huduma ya kisaikolojia wakati kwenye magazeti anaonekana hii inatupa changamoto. “Mtu anasema anatibiwa kisaikolojia lakini kila siku nikiona magazeti anaonekana anawaka, inanipa tabu.”amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amesema miongoni mwa anaohitajika kuhojiwa ni dereva wa Lissu ambaye awali viongozi wakuu wa CHADEMA walitoa taarifa na kueleza kwamba dereva huyo yupo jijini Nairobi akipatiwa matibabu ya kisaikolojia kutokana na shambulio aliloshuhudia kwa macho yake kupigwa risasi kwa  Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Pamoja na hayo IGP Sirro amewataka waandishi wa habari kuwasilisha taarifa hiyo kwa umma akisema, “Kimsingi waandishi wa habari naomba mlipeleke hili sisi tuna uchungu sana na mheshimiwa Tundu Lissu, tunamheshimu ni mtu muhimu kwa Watanzania na sisi tunataka tuwapate waliofanya lile tukio lakini ushirikiano ni mzuri ili kufanikiwa,”

Nakuongeza kwamba "Ndugu zangu, mheshimiwa Lissu amepigwa risasi na watu tunaowatafuta, huyo kijana kuja kwake kutatusaidia kupata majibu ya mambo mengi,” ameongeza IGP Sirro.



Tundu Lissu ambaye yupo Jijini Nairobi nchini Kenya  kwa ajili ya matibabu, alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na watu wasiojulikana.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search