Gazeti lingine lafungiwa na serikali kwa siku 90...Soma habari kamili na Matukio360...#share
SERIKALI imelifungia Gazeti la Tanzania Daima kwa siku 90, kwa
kile kinachodaiwa kuchapisha makala na habari zinazokiuka misingi na maadili ya
uandishi wa habari.
Gazeti la Tanzania Daima lililofungiwa kwa siku 90 na serikali.
Hayo yamebainishwa leo katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya
habari na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.
Hassan Abbas akieleza sababu za serikali kulifungia gazeti hilo.
“Hatua hii inafuatia mfululizo wa gazeti hili kucapsha habari
na Makala zenye uchuchezi, lakini vile vile zinazokiuka misingi na maadili ya
uandishi wa habari, lakini vile vile na sharia za nchi,” amesema Dk. Abbas.
Kufungiwa kwa Gazeti hilo kuna kuja baada ya serikali kuwa
imekwisha yafungia magazeti mengine ya Mwanahalisi, Mawio na Raia Mwema kutokana na
kudaia kuandika habari zinadaiwa ni za kichochezi.
Taarifa kamili ya serikali
No comments:
Post a Comment