George Bush aomba msamaha...soma habari kamili na Matukio360...#share
RAIS
mstaafu wa Marekani George Bush ameomba msamaha kwa dhihaka aliyosababisha
baada ya muigizaji, Heather Lind kumtuhumu kuwa alimnyanyasa kijinsia.
Heather Lind mwanamke anayedai kunyanyaswa kijinsia na rais mstaafu wa Marekani, George Bush
Heather
Lind amesema rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93 alimshika kutoka nyuma
akiwa katika kiti chake cha magurudumu na kutamka ''mzaha mchafu'' wakati
wakijiandaa kupiga picha.
Bi Lind alitoa madai
hayo katika mtandao wa Instagram katika chapisho ambalo limefutwa.
Hata hivyo msemaji wa
Bush amesema tukio hilo lililotokea mwaka 2014 lilikuwa jaribio la
ucheshi.
''Rais Bush alikuwa
hawezi chini ya hali yoyote ile na kwa makusudi kumsababishia mtu dhihaka na
ameomba msamaha iwapo kitendo chake cha kuzua ucheshi kilimkosea bi Lind'',
taarifa iliosambazwa kwa vyombo vya habari inasema.
Mitandao yote
ilihifadhi chapisho hilo la Lind kabla ya kufutwa. Bush alihudumu katika
kipindi cha miaka mitano kutoka 1989 hadi 1993 na ni babake George W Bush
ambaye alihudumu mihula miwili kati ya 2001 hadi 2009. Mzee huyo anaugua
ugonjwa wa kutetemeka.
No comments:
Post a Comment