Watendaji kata, vijiji wachapwa viboko, Serikali kufuta ajira zao...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
WAKULIMA
na wafugaji waliopo katika eneo la hifadhi na misitu asili wilayani Chunya
mkoani Mbeya wanawachapa viboko watendaji kata na vijiji.
Mkuu wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Rehema Madusa
Kauli
hiyo imetolewa leo na mtendaji wa kata ya Mafyeko wilayani humo, Lucas Ongara
kwenye kikao kazi cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya kilimo mwaka 2017/18 kilichohudhuriwa
na mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa.
Amesema
wanakabiliana na changamoto hiyo kutokana na makazi ya wakulima na wafugaji
kuwepo katikati ya mapori ya hifadhi na
mara nyingi wanapofuatilia wanatekwa na kucharazwa viboko.
"Tatizo
sio kamba tunashindwa kuwaondoa wavamizi
maeneo wanayoishi ni hatarishi na wana roho za kikatiri na wanauongozi wao
ambao sio wa
serikali na wana maamuzi ya kufanya lolote sasa na sisi ni binadamu tunahofia
uhai wetu,"amesema.
Ametoa
kauli hiyo kufuatia mkuu wa wilaya ya Chunya kutoa siku sita na kuwa atasitisha ajira za watendaji ngazi za kata na vijiji watakaoshindwa
kuwaondoa wakulima na wafugaji
waliovamia maeneo ya hifadhi na misitu
ya asili.
“Kuna kasumba ya
watendaji na wenyeviti wa vijiji
kuuza maeneo katika
hifadhi jambo linalosababisha serikali kuingia gharama ya kuwaondoa
wakulima na wafugaji kwa kuteketeza makazi yao.
"Siwezi
kuvumilia au kukaa na watu wasioitakia mema serikali kwa kutanguliza maslai ya
fedha mbele, Chunya imeharibiwa katika maeneo ya hifadhi. Natoa siku sita muwaondoe wote waliovamia maeneo ya hifadhi. La
Sivyo nitasitisha ajira za watendaji wa kata na vijiji.” amesema
Pia amewaagiza
watendaji kuhakiki vijiji hewa visivyokuwa katika mpango wa matumizi bora ya
ardhi na idadi ya wakulima ili kufanya tathimini ya mahitaji hususan upatikanaji wa pembejeo za kilimo na kuwaingiza
katika vijiji vinavyotambuliwa kisheria .
Kaimu Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Chunya, Ester Mwakalile ameahidi kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo na kuonya watendaji
na wenyeviti wa
vijiji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujilimbikizia mali kupitia migongo ya
wakulima na wafugaji .
Mkulima
wa kijiji cha Sangambi, Athanas Mabul amesema hawapingani na serikali ila
viongozi wa ngazi za kata na vijiji wanawachangisha fedha kwa madai zinapelekwa
serikali hali inayopelekea kwenda katika maeneo ya hifadhi.
No comments:
Post a Comment