Hatimaye Kitila Mkumbo Amkimbia Zitto Kabwe ..Ni Rasmi Ajiondoa ACT-Wazalendo..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share




KATIBU  Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambaye pia alikuwa Mwananachama wa Chama cha ACT-Wazalendo Profesa Kitila Mkumbo ameandika barua ya kujivua uanachama wa ACT Wazalendo kuanzia leo.

Itakumbukwa kabla ya kuteuliwa na Rais John Maagufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Mshauri wa chama hicho kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo na kuamua kubaki kama mwananchama wa kawaida.

Kwa mujibu wa barua ambayo Profesa Mkumbo ameandika Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Act-Wazalendo,Dorothy  Semu, amesema sababu iliyomsukuma kuachana na chama hicho ni kutokana na kukwepa mgongano wa kimaslahi katika kuitumikia serikali ya Chama cha Mapinduzi wakati huo huo  akiwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.

BARUA KAMILI HIYO HAPO



Kuibuka kwa Taarifa hii ya Profesa Mkumbo kuna kuja ikiwa ni miezi mitatu kupita baada ya Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu kumvaa msomi huyo kwa kusema kuwa alikuwa kwenye vyama vya upinzani kwa kazi moja ya kuua upinzani ili kukisaidia chama cha CCM kiendelee kubaki madarakani.

Profesa Mkumbo ambaye kabla ya kuhamia chama cha Act-Wazalendo alikuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambapo alifukuzwa kweye chama hicho kikuu cha upinzani nchini baada ya kutuhumiwa   kuwa alikuwa anapanga mipango kwa kushirikiana na watu wa usalama kwa ajili ya kuandaa mkakati wa kumvua mwenyekiti wa chama cha Chadema ,Freeman Mbowe.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search