Mbowe Amshambulia Askofu Pengo..Ni Kauli Yake Juu Ya Katiba Mpya..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
MWNYWKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani
na nje ya kanisa.
Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni
kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba,
imetushangaza na imenisikitisha.”
Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu
yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema
haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba
uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”
Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama
ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.
“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande
zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema
Mbowe.
Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli
iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine
Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni
yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.
Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu
iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na
kauli ya Askofu Niwemugizi.
“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa
kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa
kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.
Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya
habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza
yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.
No comments:
Post a Comment