Homa Ya Ini Yaendelea Kuwa Tishio..Soma Habari Kamili na Matukio360...#share

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .
003
Daktari Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
Akitoa taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam,  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema  muamko ni mkubwa  ambapo katika kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili wagonjwa  950 .
Akifanunua amesema  hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi  ya wagonjwa itaongezeka na kufika   1800  .
Hata hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi , nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni  wagonjwa 40.
‘’Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika wagonjwa 1800  lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa  hawa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi  ili aanze kutumia dawa lakini  si wote wanaohitaji dawa’’ amesema DK. Rwegasha.
Kwa upande wake Dk. Tuzo Lyuu amesema tatizo la ugonjwa huo ni kubwa kwani tafiti ambazo zimefanyika ,  watu wanaoenda kuchangia damu asilimia nane wanatatizo hilo na kusisitiza kuwa tatizo hilo si la Tanzania pekee bali  hata kwa nchi zingine zinazoendelea.
Kwa mujibu wa Dk. Lyuu kwa sasa tatizo la Homa ya Ini (Hepatitis B) ni kubwa kuliko Ukimwi .
‘’ Hapa MNH watu tunaowaona ni vijana na watu wazima na wanaume ndio wengi ingawa hakuna takwimu halisi’’ amesema Dk. Lyuu.
Ugonjwa wa Homa ya Ini unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na maambukizi ya ugonjwa huo yanashabiana na njia ya  maambukizi ya Vrusi vya  Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama, kuchangia sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.
001
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa mengine.
002
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.

004
Madaktari bingwa, wauguzi na watumishi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Dk Rwegasha leo.
005 A
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Priumus Saidia akizungumza kwenye kongamano hilo leo.
005 B
Baadhi ya madaktari, wauguzi wa hospitali hiyo na watumishi wengine wakiwa kwenye kongamano hilo leo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search