IGP Sirro Ataka Wakwepa Kodi Wachukuliwe Hatua Kali..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro ameagiza wafanyabiashara na watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi nchini kuchukuliwa hatua kali kwani wanarudisha nyuma na kuchelewesha maendeleo ya nchi.
IGP Sirro amesema hayo jana alipofanya ziara mkoani Mbeya na kuwaagiza askari wa vikosi mbalimbali vya polisi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi.

"Kuna watu wanafikiri ni sifa kufanya magendo wote tunajua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyo tumepanga mpango mkakati wa kuwashughulikia vizuri sana wale ambao wanakwepa kulipa kodi, wananchi wetu wanapaswa kubadilisha mtazamo wao waone wanawajibika kwenye kulipa kodi sababu kodi ndiyo inafanya maendeleo ya nchi yetu, kodi ndiyo inaleta madawa, kodi inaleta barabara na kodi ndiyo kila kitu. Na wale ambao wanakwepa kulipa kodi nimetoa maelekezo kuwashughulikia kila mahali na kila siku wanasikia Amiri Jeshi Mkuu anazungumzia habari hii sasa wewe unayekwepa kulipa kodi ni nani" alisisitiza Sirro

Aisha IGP Sirro aliwataka wafanyabiashara pamoja na wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kupata maendeleo na kusonga mbele zaidi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search