Watu nane Wafariki Kufuatia Gari Kutumbukia Ziwa Viktoria..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

WATU nane wamefariki huku wawili wakiokolewa wakiwa salama baada ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi jijini Mwanza.
Ni Mapema leo Juhudi za kuopoa miili ya watu waliokuwemo kwenye gari hiyo zikifanyika.
Akizungumza leo na chombo kimoja cha habari nchini, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali wakilishuhudia tukio hilo la kuzama kwa gari ndogo ya abiria (HIACE),ambalo  namba zake za usajili hazikuweza kutambulika mara moja,mara baada ya kuopolewa ziwani.
Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.
Wananchi kutoka maeneo mbali mbali wakilifuatilia tukio hilo mapema leo Kigongo Feri jijini Mwanza
“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search