IGP Sirro Awacharukia Wanasiasa..Atoa Kauli Hii Dhidi Yao..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
MKUU wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amewataka wanasiasa nchini kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwa ni pamoja na upelelezi unaoendelea wa tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chma cha Mawakili Tanganyika (TLS) Tundu Lissu.
IGP Sirro amesema hayo siku moja baada ya viongozi mbalimbali wa upinzani kutoa kauli kuhusu jeshi hilo la polisi na kusema kuwa hawana imani na uchunguzi ambao unafanywa na jeshi hilo dhidi ya tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Godbless Lema wa Arusha pamoja na Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini ni kati ya wabunge ambao walionyesha kusikitishwa na kauli ambayo aliitoa IGP Sirro akiwa mkoani Mtwara kuhusu uchunguzi wa sakata la Tundu Lissu na kusema kuwa dereva wa Lissu anachelewesha upelelezi wa sakata hilo.
Wabunge hao walikwenda mbali zaidi na kusema wao wanaona jeshi la polisi halihitaji kufanya uchunguzi wa kina juu ya sakata hilo kwa kuwa jeshi hilo linafahamu nini kipo nyuma ya tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma. Kufuatia kauli hizo IGP ndipo amefunguka na kuwataka wanasiasa kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwa pamoja na uchunguzi wa sakati hilo.
No comments:
Post a Comment