AREPEB Lazindua Mfumo wa Kielekroniki Kukusanya Maoni ya Ukuzaji wa Amani..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya ukuzaji wa amani, utoaji elimu kwa umma, haki za binadamu, misingi ya utawala bora, usuluhishi wa migogoro na kutoa mijadal ya amani (AREPEB), limezindua mfumo wa kielektroniki unaotumika kukusanya maoni juu ya ukuzaji wa amani ya nchi.
 Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Bi. Imelda Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika hilo Yohana Mcharo na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.

Aidha, limesema linatarajia kuzindua mafunzo yatakayojadili amani na utatuzi wa migogoro pamoja na Haki za Binadamu na msisingi ya utawala bora yatakayofanyika Kibaha mkoani Pwani Oktoba 7 hadi 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa AREPEB Imelda Mushi, amesema mfumo huo utatoa taarifa ya misingi ya utawala bora kwa kutuma ujumbe wa mamneno bure kupitia namaba 0800712121 au + 255 757 333 773 na +255758333773 bila ubaguzi wowote.

“Mfumo huu ni huru kwa wananchi wote bila ubaguzi wito wetu kwa wananchi ni kuutumia mfumo huu ili kila mwananchi aweze kuchangia ukuzaji wa amani, haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa kutuma maoni” amaesema Mushi.

Ameabinisha kuwa ushauri na maoni yatayotolewa ama kukusnaywa yatafanyiwa  na kuapata taarifa muhimu ambazo ziataumika kushauri mamalaka husoika ili kuchukua matakwa hatua za kufikia matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu kuheshimu amani iliyopo, haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Amesisitiza kuwa AREPEB inatekeleza maradi wa amani, haki za binadamu na utawala bora kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS) utakaofanyika kwa kipindi cha miezi sita mwezi Agosti hadi Oktoba mwaka huu na mwakani kuanzia Februari hadi Machi.
Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Yohana Mcharo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, katikati ni Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Bi. Imelda Mushi na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.
Na Hussein Ndubikile

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search