JPM Awatosa Mawaziri Wake Wanne..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

WAKATI mapema leo Rais John Magufuli akifanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri, mabadiliko hayo yamewaweka pembeni Mawaziri wanne ambao walikuwemo katika baraza la kwanza. 

Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi,  Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search