LHRC Yaitaka Serikali Kufuta Adhabu ya Kifo...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

Na Abraham Ntambara
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka
serikali kubadilisha sharia, kuondoa adhabu ya kifo kwa kuweka adhabu mbadala
kwenye makosa ya jinai na wafungwa waliopo katika vifungo vya muda mrefu
gerezani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa LHRC Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupinga adhabu ya kifo leo jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga akizungumza na Mtandao wa Matukio360,
amesema kuwa kituo hicho kinaungana na Mtandao wa Kupinga Adhabu ya
Kifo Duniani katika maadhimisho ya 15 siku ya kupinga adhabu ya kifo.
Henga amesema adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili ambayo
inakinzana na misingi ya utu na haki za binadamu kama ilivyoainishwa katika
mikataba mbalimbali ya kimataifa.
“Adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili isiyo ya staha,
inayotweza utu wa binadamu, inafanya serikali ionekane pia kama mhalifu kwa
kuua, tuitake serikali ibadilishe sharia na kuondoa adhabu ya kifo na kuweka
adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vifungo vya
mrefu,” amesema Henga.
Aidha LHRC kime mpongeza Rais John Magufuli kwa kuweka wazi
msimamo wake wa kutounga mkono adhabu ya kifo kwani ni ya kinyama na
isiyostahili binadamu yeyote.
Kwa upande mwingine Henga ametoa sababu za kituo hicho kupinga adhabu hiyo. Miongoni
mwa sababu hizo ni pamoja na adhabu kuwa ya kibaguzi kwani mara nyingi
wanaopatikana na hatia na kupewa adhabu hiyo ni maskini wasioweza kuwa na
ushauri wa kisheria na watu wengine.
Nyingine ni vigumu kuthibitisha kuwa inatekelezwa tu kwa watu
ambao wametenda na kukutwa na hatia ya kosa hili au wabaya Zaidi, Adhabu hiyo
ikitolewa kwa mtu asiye na hatia kimakosa huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa
utoaji haki huwa pia na uwezekano wa kuwa na mianya ya makosa.
Ameongeza nyingine kuwa ni adhabu kutompa nafasi mtuhumiwa
kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi na wala haimsaidii mtu yeyote hata
familia ya muathirika, hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inazuia watu
wengine kutokwenda makosa kama hayo.
No comments:
Post a Comment