MAGUFULI: NILITINGISHWA amtunuku tuzo Ndugai, Paramagamba...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
RAIS Dk John Pombe Magufuli amesema hatua yake ya kupambana na kudhibiti madini nchini ilimtingisha lakini alisimama imara kwa manufaa ya watanzania na vizazi vijavyo.
Rais Dk Jonh Pombe Magufuli
’Hata mimi nilipoanza kupambana na kudhibiti madini mtikisiko niliokuwa naupata niliujua mwenyewe lakini nikasema nitapambana hadi hatua ya mwisho kwa ajili ya watanzania na vizazi vyetu.’ amesema Rais Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatunuku vyeti vya shukran na pongezi wajumbe 27 wa kamati ya almasi na dhahabu na Tanzanite katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Pia amemuagiza waziri wa katiba na sheria, Profesa Paramaganda Kabudi kuakikisha sheria ya Takwimu inafanya kazi ili kudhibiti wanaopotosha takwimu za nchi kwa makusudi ikiwamo kufikishwa Mahakamani.
Amesema tayari thamani ya Tanzanite imeanza kupanda katika soko la Dunia na kwamba hiyo inatokana na udhibiti wa madini hayo.
‘Lengo la wasema hovyo kuhusu serikali ni kutaka kuichonganisha na wananchi lakini tumesimama na kudhibiti hali hii kwa sababu ya watanzania.’ amesema
Rais amesema kupitia udhibiti huo serikali imeweza kuendesha miradi mbalimbali ikiwamo ya ununuzi wa ndege sita, ujenzi wa barabara, ujenzi wa reli bila kutegemea misaada kutoka kwa wahisani.
Amewatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick.
Mbali na Spika wa Bunge Job Ndugai wajumbe hao ni Profesa Kabudi, Prof Abdulkarim Mruma, Yamungu Kuyabila, Geofrey Mwambe, Adolf Ndungulu,Prof Andrew Luoga, Kasimilia Kiuki, Andrew Massawe, Saje Kasibisye, Adejeni Mwaipopo, Tedi Sikuluwasha, Moses Edward Moses.
Wengine ni John Lianga, Andrew Mwangakara, Michael Kambi, Professa Kiyalunzi, Dk Osward Mashinana, Gabriel Malata, Butamo Philip, Profesa Justinean Lutangwira, Professa Lwegasira, Dk Athuman Ngenya, Dk Joseph Philip, Dk Amlosi Itika, Muhamed Makongoro na Henry Gombela
Oktoba
19,2017, Tanzania na Barrick Gold
Cooperation zilifia makubaliano na kutialiana saini mkataba wa kutekeleza
mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya
dhahabu yaliyochimbwa katika migodi yake nchini pamoja na kulipia takribani
Dola za kimarekani bilioni 700 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya
upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.
No comments:
Post a Comment