Professa Luoga gavana mpya BoT..soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
RAIS Dk John Pombe Magufuli amemteua Professa Andrew Luoga kuwa gavana mpya wa Benki kuu ya Tanzania(BoT).


Professa Andrew Luoga Gavana mpya wa Tanzania(BoT)
Ametangaza uteuzi huo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatunuku vyeti vya shukran na pongezi wajumbe 27 wa kamati ya almasi na dhahabu na Tanzanite katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Amesema hatua yake hiyo inafuatia gavana wa sasa Profesa Benno Ndullu kumaliza muda wake wa utumishi wa umma ifikapo Desemba mwaka huu, au Januari, 2018.

‘Kwa kweli gavana Professa Ndullu amefanya kazi kubwa lakini muda wake wa utumishi unaishia Desemba au Januari, 2018 hivyo nimemteua Profesa Luoga kuwa gavana mpya mara tu baada ya Ndullu kuondoka.’

Amesema ‘ Najua watu watasema nimechagua gavana ambaye si mchumi lakini manaibu wake ni wachumi hivyo sioni tatizo lolote katika hili mpeni ushirikiano wa dhati katik utendaji wake.’


Pia amemuagiza waziri wa katiba na sheria, Profesa Paramaganda Kabudi kuakikisha sheria ya Takwimu inafanya kazi ili kudhibiti wanaopotosha takwimu za nchi kwa makusudi ikiwamo kufikishwa Mahakamani.

‘Upotoshwaji wa takwimu unaathiri nchi mfano mwekezaji anapopata takwimu zisizosahihi inapelekea ashindwe kuwekeza nchini hivyo tuwe makini na utoaji wa takwimu na pia tuangalie uzalendo.’


Amewatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick.

Mbali na Spika wa Bunge Job Ndugai wajumbe hao ni Profesa Kabudi, Prof Abdulkarim Mruma, Yamungu Kuyabila, Geofrey Mwambe, Adolf Ndungulu,Prof Andrew Luoga, Kasimilia Kiuki, Andrew Massawe, Saje Kasibisye, Adejeni Mwaipopo, Tedi Sikuluwasha, Moses Edward Moses.

Wengine ni John Lianga, Andrew Mwangakara, Michael Kambi, Professa Kiyalunzi, Dk Osward Mashinana, Gabriel Malata, Butamo Philip, Profesa Justinean Lutangwira, Professa Lwegasira, Dk Athuman Ngenya, Dk Joseph Philip, Dk Amlosi Itika, Muhamed Makongoro na Henry Gombela


Oktoba 19,2017,  Tanzania na Barrick Gold Cooperation zilifia makubaliano na kutialiana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yaliyochimbwa katika migodi yake nchini pamoja na kulipia takribani Dola za kimarekani bilioni 700 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search