Mahakama Yashindwa Kutoa Uamuzi Kesi ya Wema ...Soma Habari Kamili na Matukio360...#share

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi wa ama kupokea au kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu Hakimu hajamaliza kuandaa uamuzi huo.

Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo October 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi November 1, 2017.

Awali, Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba Mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.

Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search