Mbeya kuhakiki vyeti vya maafisa ugani...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Mwandishi wetu
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amemwagiza kaimu katibu Tawala Mkoa, Costantine
Mushi kufanya uhakiki wa vyeti kwa
maofisa ugani kuanzia ngazi ya kata,kijiji na halmashauri ili kubaini wanaostahili kuwepo katika ajira
serikalini
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
Makalla
ametoa agizo hilo kwenye kikao maalum cha kazi kilichohusisha wakuu wa wilaya,
wakurugenzi, wakuu wa idara, maofisa kilimo na mifugo wa halmashauri wakati wa kikao cha kazi cha
kujadili
mikakati
ya kuboresha sekta ya kilimo mwaka 2017/18.
Amesema kuna kasumba ya maofisa ugani kutojua
majukumu yao sehemu za kazi hali inayosababisha kutoa takwimu za uongo za uzalishaji
wa mazao ya chakula na biashara
"Nimebaini wapo
maofisa ugani ambao hawana sifa
sasa katibu Tawala haraka anza zoezi la
uhakiki wa vyeti kabla ya msimu wa kilimo haujaanza. Lengo la Serikali ni kuwa
na wataalam wanaowafikia wakulima vijijini na
si kukaa maofisini. "amesema.
Aidha
ameonya maofisa kilimo na mifugo katika halmashauri zote kuacha kufanya kazi
kwa mazoea na kushindwa kusimamia majukumu yao na kuwa
Ni
bora serikal ibaki na watu wachache wanaotambua majukumu yao na si kuwa na idadi kubwa ya watumishi
wanaopata mishahara ya bure .
Naye
Ofisa Kilimo Mkoa wa Mbeya, Enock Nyasebwa amesema mkoa umeweka lengo la kuzalisha tani 3.9 za mazao ya chakula na biashara mwaka
2017/18.
Pia
kutoa elimu kwa maofisa ugani na wakulima ili
kufikia
lengo walilokusudia la kuzalisha mazao yaliyo na tija katika kuelekea uchumi wa
viwanda.
Akizungumza kwa niaba
ya wakuu wa wilaya, mkuu wa wilaya ya Rungwe, Julius Chalya amesema watatekeleza agizo la mkuu wa mkoa, kwa
kuanza uhakiki ili kuiwezesha Serikali kupata wataalam watakayoifikisha Tanzania
katika uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment