Rais mstaafu Goodluck Jonathan aitwa mahakamani .Soma habari kamili na Matukio360..#share

JAJI wa Mahakama Kuu nchini Nigeria ameamuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan apewe hati ya kuitwa mahakamani kuhusu kesi ya rushwa inayomkabili msemaji wake wa zamani katika chama cha Peoples Democratic Party (PDP).
Rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan

Hatua hiyo inatajwa kama ya kushangaza na ambayo itafuatiliwa kwa karibu kutokana na  kwamba Jonathan amekuwa akitajwa katika matukio mengi ya kifisadi japokuwa hakuwahi kuitwa na kuhojiwa rasmi.

Msemaji wa zamani wa rais huyo, Olisa Metuh anakabiliwa na kesi anayoshtakiwa kwa kosa la kujipatia kwa njia za udanganyidui dola 1.1 milioni za Marakeni kutoka kwa Sambo Dasuki mshauri wa masuala ya usalama wa Jonathan.

Katika utetezi wake, msemaji huyo ameng’ang’ania kwamba alipokea fedha hizo kwa maelekezo yaliyotolewa na Jonathan ili kugharimia kampeni za kutetea kiti chake mwaka 2015.

Jumatatu, mawakili wa Metuh walisema kwamba wanakusudia kumwita rais huyo wa zamani kama shahidi.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho Abang Okon anayesikiliza shauri hilo alisema itakuwa “sawa na ukiukwaji wa haki zake (Metuh) kwa usikilizwaji wa haki ikiwa hatatia saini hati ya kuitwa mahakamani".



"Sina chaguo jingine zaidi ya kutia saini hati ya mahakama ya kumlazimisha rais wa zamani Goodluck Jonathan kufika mahakamani jana Oktoba 25, 2017 ili aweze kutoa ushahidi wake," amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search