Mbunge Arusha Mjini Godbless Lema Anusurika Ajali kwa Mtego wa Watu Wasiojulikana..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


GARI la Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema  limechomoka matairi leo Jumatatu baada kudaiwa kuwa limefunguliwa nati 13 kati ya 20 na watu wasiojulikana.
Lema amesema walikuwa wamepanga na Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema), Joshua Nassari kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema.

Hata hivyo amesema majira ya mchana alipokuwa na gari alihisi mlio kwenye tairi ndipo alikwenda kuliegesha hoteli ya Equator.

Amesema kutokana na kulitilia shaka gari aliomba lifti kwenye gari la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph kwenda naye Dar es Salaam.

"Asubuhi leo (Jumatatu) nikamtuma dereva wangu akachukue gari Equator hoteli alipeleke gereji na baada ya kutoka mita chache tairi zilichomoka," amesema.

Amesema tayari amemuagiza dereva kwenda kutoa taarifa polisi lakini ameiomba kampuni ya  ulinzi ya inteligence inayolinda nyumba yake kufanya uchunguzi kubaini watu walioingia ndani na kufungua nati.

"Pia nimeomba wataalam kupitia kamera za nyumbani kwangu kuona kilichotokea kwani kuna uwezekano wa watu kuingia ndani kufanya uhalifu huo.”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search