Wabunge Nassari, Lema Chadema Watinga Takukuru...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki na Godbless Lema wa Arusha Mjini wamefika leo katika Makao makuu ya ofisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Jijini Dar es Salaam kukabidhi kile wanachokiita ushahidi unao onesha jinsi baadhi ya madiwani wa chama hicho mkoani Arusha walivyorubuniwa kwa Fedha hadi kujizuru nyadhifa zao.
Wabunge hao wamefika Takukuru wakiwa wameambatana na Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa.
Itakumbukwa jana wabunge hao wakizungumza na waandishi wa hababari walitoa ushahidi huo na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.
Katika ushahidi huo viongozi kadhaa wamerekodiwa wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa miradi yao.
Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi.
Itakumbukwa pia Wakati wabunge hao wakifanya wakifanya hivyo ni kwamba tayari baadhi ya madiwani waliojiuzulu walisema kuwa hawakushawishiwa na mtu yeyote wala kupewa rushwa bali wamehama kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.
No comments:
Post a Comment