Mkurugenzi Chadema, Benson kufikishwa Mahakamani...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
MKURUGENZI
wa Operesheni na Mafunzo wa chama cha Chadema, Kigaila Benson uenda kesho akafikishwa
Mahakamani kwa madai ya kutoa lugha ya uchochezi
na kashfa.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa
Chanzo
chetu kutoka Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kimesema Benson
alitakiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ijumaa iliyopita
lakini ilishindikana.
‘NI
uhakika kesho Jumatatu, Kigaila Benson atafikishwa katika mahakama ya kisutu
kujibu mashtaka yanayomkabili. Ilitakiwa afikishwe Ijumaa iliyopita lakini
kutokana na sababu kadhaa ikashindikana,’ kimesema chanzo chetu hicho
Hivi
karibuni Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa alithibitisha kukamatwa
kwa Mkurugenzi huyo kwa mahojiano kwa madai ya kutoa lugha ya kuikashfu
serikali na watu wake.
Alisema
"Tunaendelea kumshikilia na anaendelea kuhojiwa atakapokamilisha yale
ambayo yanamuhusu tutaelekeza kesi mahakamani kama ushahidi utakuwepo wa
kutosha,"amesema.
Mambosasa
amesema endapo ushahidi utakuwa wa kuendelea na mashahidi wengine wataangalia
kupata dhamana huko mbele kwani jeshi hilo halijakamilisha yale waliokusudia.
No comments:
Post a Comment