Zitto 'kuidadavua' serikali leo...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na mwandishi wetu
CHAMA cha ACT Wazalendo leo kinazindua  kampeni zake rasmi  za kugombea nafasi ya udiwani katika kata 43 nchini.


Zitto Kabwe  ambaye ni kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo akiwa katika moja ya mikutano ya  hadhara ya kampeni
Afisa habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamis ameiambia Matukio360 kuwa kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe atazindua kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam katika kata ya Kijichi.

Pia viongozi wengine wa kitaifa watakuwapo na kwamba mgombea wa udiwani wa kata hiyo wa ACT Wazalendo, Mkosamali Edga anayetarajia kupambana na   vyama vingine ikiwamo  CCM na Ukawa, atatambulishwa rasmi

Uchaguzi huo mdogo wa marudio wa udiwani utafanyika Novemba 26, 2017, utahusisha kata 43 nchini, Dar es salaam ikihusisha kata ya Mbweni, Kijichi na Saranga

Akunukuliwa jana Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma mjini amesema utafiti walioufanya unaonyesha chama hicho kinaweza kuchukua kata za Kijichi na Saranga endapo vyama vingine vya upinzani vitakiachia ACT Wazalendo.

 Mkutano huo utafanyika katika viwanja vya Centre Kijichi kuanzia majira ya saa tisa Alasir

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search