Mshambuliaji wa Zamani Arsenal Ian Wright Ataja Mrithi wa Wenger..Soma Habari Kamili na Matukio360...#share
Klabu ya Burnley kwa
sasa katika msimamo wa ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) wanashika nafasi
ya sita baada ya kuifunga Evertoni nyumbani kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.
Baada ya kujiunga na Klabu ya Lancashire mwaka 2012, Dyche ameweza
kuiongoza Burnley kwa misimu miwili kwa michezo ya kupanda ligi kuu na waliweza
pia kushuka daraja misimu mitano iliyopita.
"Nina amini yeye
(Dyche) ni mtu fulani ambaye anahiaji kupiga hatua hatua fulani, katikamhatua
nyingine,” Wright ameiambia BBC Radio 5 live.
"Ni kocha mwenye uzoefu katika Premier League. Ameshafanya
kazi nzuri na timu ndogo na zimeweza kufanya vizuri,”. Ameongeza.
Arsene Wenger aliongeza mkataba wa miaka miwili mwezi wa Juni
mwaka huu baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuhusu kuendelea au kutoendelea
kuifundisha klabu ya Arsenal.
Wright alipoulizwa kama Dyche anafiti kuirithi mikoba ya Wenger Arsenal, alijibu: "Ndiyo. Je ukweli ni
kwamba watampa Sean Dyche kazi hiyo?
"Kwa kuheshimu namna alivyoitengeneza timu yake jinsi
wanavyo ziuia, ni wazi yuko vizuri, lakini je atapewa kazi kama hiyo? Si fikiri
kama atapewa.
No comments:
Post a Comment