Daktari: Elimu ya ngono itolewe shuleni...soma habari kamili na matukio360...#share


 Na Mwajuma Kombo, Zanzibar
SERIKALI imeshauriwa  kutoa elimu ya ngono shuleni ili watoto waweze kujua athari za kufanya mapenzi wakiwa na umri mdogo. 
Dk Marijani Msafiri

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt Marijan Msafiri wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kutaka kujua mambo mbali mbali kuhusu athari zinazopatikana kuhusu kufanya mapenzi utotoni.

Amesema hatua hiyo pia itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mimba za utotoni

Dk. Marijani ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama katika Hospital ya Rufaa ya Mnazimmoja amesema kuwa hili ni shauri lenye malengo mazuri hasa ikizingitiwa kuwa wengi wa watoto wamekuwa wakishiriki mapenzi wakiwa hawajui athari yake.

"Kumekuwa na wimbi kubwa la mimba za utotoni ambao wengi wao wanafanya wakiwa hawajui lakini ni lazima elimu ya ngono kutolewa mashuleni kwa wanafunzi ili watoto waweze kujua athari ya kufanya mapenzi wakiwa na umri mdogo, " amesema.

“Lengo sio kuwafundisha kufanya ngono bali elimu hii watoto kuweza kujua athari za mimba za utotoni na unapofanya kitendo cha ndoa wakati bado umri ni mdogo kunamadhara yanaweza kujitokeza.”aliongeza.

Amesema iwapo elimu hiyo itatolewa mimba za umri mdogo zitapunguwa ikiwemo na maradhi.

Pia amesema njia nyingine ili kupunguza vitendo vya    udhalilishaji ni jamii kurejea katika malezi ya zamani ya kuwajali na kuwahurumia watoto.

Alisema utamaduni wa zamani watu walikuwa wakiishi kwa upendo huku kila mzazi anao uhuru wa kumlea mtoto wa mwezake katika kumuongoza katika mambo mema na kumkataza mabaya.

“Hivi sasa watoto hawalelewi na jamii nzima lakini pia akinababa wamesahau wajibu wao na mzigo wa malezi wameachiwa wanawake pekee,”amesema.

Amesema watoto wengi hivi sasa hawana uwangalizi hali ambayo imepelekea wabakaji kuweza kupata mwanya wa kuwadhalilisha watoto.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search