Ndege yaanguka na kujeruhi 11...Soma habari kamili na Matukio360..#share
MAPEMA mchana wa leo ndege aina ya Cessna Grand Caravan ikiwa
na abiria 11 na Rubani imeanguka ikiwa angani maeneo ya Mbuga ya Serengeti.
Katika ajali hiyo abiria wawili na rubani ambao walipata majeraha makubwa, walisafirishwa
kwenda Nairobi kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu kwa msaada wa watu wa
Coastal huku waliobaki wakipata majeraha
madogo madogo.
Kwa Mujibu wa Mkurugenzi, Julian Edmunds, ambaye alikuwemo
katika ndege hiyo ambayo ilikuwa imetokea Nairobi nchini Kenya, ameeleza kuwa
miongoni mwa majeruhi hakuna ambaye alipata majeraha yakutisha.
Inasemekana ajali hiyo imechangiwa na mvua ambayo ilifanya rubani ashindwe kuona vizuri hivyo Wakati
anajaribu kutua akajikuta ameshafika katikati ya uwanja hali iliyomfanya apitilize
na kugonga miti na mawe.
No comments:
Post a Comment