UDART yasimamisha usafiri mabasi ya mwendo kasi...Soma habari kamili na Matukio360..#share
KAMPUNI inayotoa huduma kwenye mradi wa mabasi yaendayo
haraka UDART, imetangaza kusitisha huduma hiyo kuanzia mchana mchana wa leo.
Basi la usafiri wa haraka ya UDART
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na Deus Bugaywa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, amesema sababu za kusitisha huduma hiyo
ni kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro baada ya daraja la mto Msimbazi
kujaa maji.
“Tunaujulisha umma kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda
kuanzia saa 7:30 mchana wa Alhamis Oktoba, 26, 2017, kutokana na kufungwa kwa
Barabara ya Morogoro kwa sababu ya daraja la mto Msimbazi kujaa maji,” imesema
taarifa hiyo.
Aidha imeeleza kuwa huduma itarejea mara baada ya hali
kutengemaa, hivyo kutokana na hali hiyo kampuni imeomba radhi abiria kwa
usumbufu uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment