Ni Cristiano Ronaldo tena...soma habari na Matukio360...#share
CRISTIANO
Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka FIFA la mchezaji bora wa kiume wa
mpira wa miguu mwaka 2017 ikiwa ni mara ya
pili mfululizo.
Mchezaji soka,Christiano Ronaldo
Mchezaji
huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka,
kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliochangia
kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na ligi ya
mabingwa Ulaya - Champions League.
Ronaldo
aliyepata watoto mapacha hivi karibuni alipokea
tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji
wenzake, kocha na rais wake.
Tuzo
hiyo kwa mchezaji bora mwanamke imenyakuliwa na mchezaji wa Uholanzi Lieke
Martens, anayeichezea Barcelona.
Aliwahi
pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017.
Ronaldo ambaye pia alikumbwa
na kashfa ya ukwepaji kulipa kodi amewashinda wachezaji Messi wa Barcelona na
Neymar wa PSG
No comments:
Post a Comment