Ni Mwaka wa 'Majanga' kwa Mfanyabiashara Yusuf Manji...TRA Nao Wamsurubu...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

UNAWEZA kusema mwaka huu ni mwaka umekuwa wa majanga kwa Mfanyabiashara na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji kutokana na kuwa na misuguano isiyokwisha na Serikali ya Awamu ya Tano na hii ni kutokana na leo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzifunga ofisi za kampuni yake kwa kudaiwa kodi ya  Sh. biloni 12.2.



Akibainisha taarifa hizo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema wamekuwa na mawasiliano na kampuni ya Farm Equpment ambayo inamilikiwa na Manji tangu Agosti 15 mwaka huu lakini kulikuwa hakuna mrejesho kuhusu deni hilo.

Kutokana na hilo amesema wamefunga ofisi zake kwa sababu kampuni hiyo inadaiwa kiasi cha Sh 12.2 bilioni lakini kampuni hiyo ina nafasi ya kuendelea kuwasiliana na TRA namna ya kulipa deni hilo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu kati ya saa 4 hadi 7 wakati TRA na kampuni ya udalali ya Yono wakiambatana na polisi walipokwenda katika jengo hilo lililopo barabara ya Pugu, wilayani Temeke.

Baadhi ya mashuhuda wakiwamo walinzi kwa masharti ya kutotaja majina yao  wamesema kuwa ofisi zilizofungwa ni ya Manji na sehemu yake duka la kuuza pikipiki na matrekta.

Wamesema baada ya kufika watu waliingia moja kwa moja katika ofisi yake kisha kufanya majadiliano na wahusika yaliyodumu zaidi ya saa 2.

"Nadhani hawakufikiana mwafaka kwa sababu walivyotoka wakaamuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kutoka nje kisha kuweka utepe wa rangi nyekundu na nyeupe," amesema shuhuda huyo.

Hata hivyo, mashuhuda hao wamesema hawajui tatizo ni nini lakini waliwasikia maofisa wa TRA na kampuni hiyo ya udalali wakizungumza kuhusu kodi.

Itakumbukwa kuwa Mfanyabiashara huyo amekuwa akikumbwa na misukosuko mingi ambayo kwa namna moja ama mingine imeweza kufanya atikisike kibiashara. Miongoni mwa misukosuko hiyo ni kutajwa katika orodha ya wanaojihusisha na dawa za kulevya hali iliyosababishwa hadi sasa kukabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa hizo ambayo iko mahakamani ikisubiri kutolewa hukumu Oktoba 6 mwaka huu.

Mingine ni kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kutokana na ghara lake lakuhifadhia mizigo kukutwa limehifadhi Vitambaa vya nguo za Jeshi la Wananchi Watanzania (JWTZ) pamoja na mihuri lakini bahati nzuri kesi hiyo imekwisha baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo hivyo kufutwa.

Siyo hiyo tu hivi karibuni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilimfuta Udiwani wa Mbagala kwa kushindwa kuhudhuria vikao vya madiwani vya halmashauri hiyo.

Na Mwandishi wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search