Diamond Platnumz arejesha fadhila alipozaliwa.. akabidhi vifaa tiba vya sh. Mil. 4
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasib Abdul, maarufu kama Diamond Platnum amesherehekea siku yake ya kuzaliwa jioni hii, kwa kutembelea hospitali ya rufaa ya Amana.
Katika kusherehemea sikuku yake ya kuzaliwa, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.
Diamond amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo sehemu alipozaliwa.
"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"
Kwa upande wake, kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Shani Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.
Dk Mwakaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.

No comments:
Post a Comment