Sports News: Ratiba ya kombe la Azam sport federation cup 2017-18 yatolewa...Soma habari kamili na Matukio360..#share
MICHUANO ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), imezinduliwa leo Jumatano Oktoba 25, 2017 kwa droo maalumu ya timu zitakazofungua dimba kwa mzunguko wa awali.
Droo hiyo imefanyika jijini Dar es
Salaam chini ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
Madadi amesema: “Michuano ya msimu
huu itaanzia hatua ya awali kabla ya kuja kwa raundi ya kwanza.”
Amesema kwa ujumla tu, michuano hiyo
ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, itashirikisha timu 91 msimu
huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); 24 za
Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya
Mabingwa wa Mkoa (RCL).
Kwa kuanzia hatua ya awali, kundi
la timu 27 la RCL timu sita zitakazocheza mechi tatu baada ya wachezaji watatu
wa zamani wa timu ya taifa Abeid Mziba ‘Tekelo’, Boniface Pawasa na Salum Sued
‘Kusi’ kuchagua vitufe sita ili kupata timu hizo.
Timu zilizopatikana katika droo
hiyo hatua ya awali Buselesele ya Geita itayocheza na Green FC ya Songwe;
Kisarawe United ya Pwani itacheza na Silabu ya Mtwara ilihali Usamala ya Simiyu
itacheza na Sahale All Stars ya Tanga kati ya Oktoba 31; Novemba mosi au mbili.
Raundi ya Kwanza ya ASFC itaanza
Novemba 7, 8 au 9 ambako timu zilizochaguliwa kwenye droo hiyo ni kama
ifuatavyo:
Mashujaa ya Kigoma itacheza na
Mshindi kati ya Buselesele ya Geita na Green FC ya Songwe; wakati mechi
nyingine zitakuwa Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya Tabora ilihali
Bulyanhulu ya Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.
Kwa mujibu wa droo, Mji Mkuu FC ya
Dodoma imeangukia kwa Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na
Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza
na Ndovu ya Mwanza.
Changanyikeni ya Dar es Salaam
itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati Mshindi kati ya Kisarawe United
na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku Cosmopolitan ikicheza na
Ajabalo wakati Makumba FC itapambana na Green Warriors ya Kinondoni wakati
Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es Salaam huku Dar City
ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.
Michezo mingine ya hatua ya kwanza
itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na Sabasaba pia ya mjini humo
wakati Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya wakati The Mighty
Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.
Timu ya Burkina FC ya Morogoro
itacheza na Mbinga United ya Ruvuma wakati Makambako Heroes ya Njombe
itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro wakati Real Moja Moja itapambana na
African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya itacheza na African Sports
ya Tanga.
Mechi nyingine za hatua hiyo
itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na Kilimanjaro Heroes ya
Kilimanjaro; huku Stand Misuna ya Singida itacheza na Madini FC ya Arusha
ilihali AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara wakati New Generation
itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga. Bodaboda FC itacheza
na Kitayose ya Kilimanjaro
No comments:
Post a Comment