Sports News: Tenga, Karia, Lina na Marealle wateuliwa kamati za CAF...Soma habari kamili na Matukio360...#share
LEODEGAR Tenga rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameteuliwa kwenye Kamati mbili tofauti za Shirikisho la Soka Afrika CAF.
Rais wa Zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF imesema kuwa Tenga ameteuliwa kwenye Kamati za Maendeleo ya Futsal na Soka
la Ufukweni na Kamati ya Ufundi na Maendeleo.
Aidha mbali na Tenga, wengine watatu wameingizwa kwenye
Kamati za CAF akiwemo Wallace Karia amabaye ni rais wa sasa wa TFF ameteuliwa
kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika
(CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Wengine ni Kaimu Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Lina Mhando
aliyeteuliwa kwenye Kamati ya Maandalizi ya Soka la Wanawake na Dk. Paul Gaspar
Marealle aliyeteuliwa Kamati ya Tiba.
Katika Kamati Kuu, Rais ni Ahmad wa Madagascar, Makamu wa
kwanza ni Kwesi Nyantakyi wa Ghana, Makamu wa pili Constant Omari Selemani wa
DRC na Makamu wa tatu ni Fouzi Lekjaa wa Morocco, wakati mbali na Tenga Wajumbe
wengine ni Adoum Djibrine (Chad), Hani Abo Rida (Misri), Almamy Kabele Camara
(Guinea), Tarek Bouchamaoui (Tunisia), Kalusha Bwalya (Zambia), Lydia Nsekera
(Burundi), Alexander Danny Jordaan (Afrika Kusini), Amaju Melvin Pinnick
(Nigeria), Hassan Musa Bility (Liberia), Isha Johansen (Sierra Leone), Rui
Eduardo da Costa (Angola), Suleiman Hassan Waberi (Djibouti), Ahmed Yahya
(Mauritania), Moses Magogo (Uganda) na Essam Ahmed wa Misri, ambaye ni Kaimu
Katibu Mkuu.
Katika Kamati ya Futsal na Soka la Ufukweni, Tenga ni Makamu
wa Rais chini ya Rais, Moses Magogo wa Uganda na Wajumbe Virginia Mendes Da
Cruz wa Guinea Bissau, Khiba Mohoanyane wa Lesotho, Hussein Abdunnaser Ahmed wa
Libya, Abilio Espirito Santo wa Sao Tome, Oumarou Fadil wa Cameroon, Abdoulaye
Saydou wa Senegal, Ali Harred Mohamed wa Djibouti, Felix Ansong wa Ghana,
Khaled Latif wa Misri, Lombe Mbalashi wa Zambia, Mahaforona Cyril wa
Madagascar, Omega Sibanda wa Zimbabwe, Pascal da Fonseca Loforte wa Msumbiji,
Pasipononga Liwewe wa Zambia, Poobalan Govindasamy wa Afrika Kusini na Senator
Obinna Ogba wa Nigeria.
Kamati ya Ufundi na Maendelezo Tenga ni Makamu wa Rais pia,
chini ya Rais, mcheΩaji mwenzake wa zamani barani, Kalusha Bwalya wa Zambia na
Wajumbe, Adoum Djibrine wa Chad, Suleiman Hassan Waberi wa Djibouti, Malouche
Belhassan wa Tunisia, Fran Smith wa Afrika Kusini, Nasser Larguet wa Morocco,
Watson Suubi Edgar wa Uganda, Khalilou Fadiga wa Senegal, Alshelmani Abdulhakim
wa Libya, Korichi Taoufique wa Algeria, Jeremie Njitap wa Cameroun, Ilonga
Erita wa DRC, Ahmed Yussuf Fresh wa Nigeria, Ahmedou Mbourick wa Mauritanie), Hazem
Imam wa Misri na Jean Michel Bennezet.
Katika Kamati ya CHAN, Karia ni Mjumbe chini ya Rais Hassan Musa Bility wa Liberia na Makamu wa kwanza, Rui Eduardo da Costa wa Angola na Makamu wa pili, Wadie Jary na Lina kwenye Kamati ya Soka la Wanawake yupo chini ya Rais, Isha Johansen wa Sierra Leone na Makamu wake, Lydia Nsekera wa Burundi wakati Dk Marealle kwenye Kamati ya Tiba yupo chini ya Rais Adoum Djibrine wa Chad na makamu wake, Yacine Zerguini
Katika Kamati ya CHAN, Karia ni Mjumbe chini ya Rais Hassan Musa Bility wa Liberia na Makamu wa kwanza, Rui Eduardo da Costa wa Angola na Makamu wa pili, Wadie Jary na Lina kwenye Kamati ya Soka la Wanawake yupo chini ya Rais, Isha Johansen wa Sierra Leone na Makamu wake, Lydia Nsekera wa Burundi wakati Dk Marealle kwenye Kamati ya Tiba yupo chini ya Rais Adoum Djibrine wa Chad na makamu wake, Yacine Zerguini
No comments:
Post a Comment