StarTimes yaahidi kukuza mpira wa kikapu nchini...Soma habari kamili na Matukio360..#share


KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd inayodhamini Michuano ya kikapu kupitia nembo yake ya StarTimes imeahidi kuhakikisha mpira wa kikapu unakua nchini.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe akiwavalisha medali mabingwa wa StarTimes Super Cup kwa mwaka 2017

Kampuni hiyo imedhamini ligi inayosimamiwa na chama cha Kikapu Dar es Salaam (BD), RBA na sasa imedhimini Super Cup.

Akiongea katika fainali za Super Cup zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam, Makamu Rais wa StarTimes Tanzania Bi Zuhura Hanif amesema, “Kampuni ya Star Media Tanzania inayo nia ya dhati ya kushirikiana na watanzania katika kukuza kiwango cha michezo nchini na hiki ni kielelezo tosha. StarTimes Super Cup inayofikia tamati leo, ni sehemu ya pili ya udhamini wetu katika kikapu Dar es Salaam baada ya kumalizika ligi ya StarTimes RBA”.

Kwa upande mwingine kampuni hiyo ina kibali cha kuonyesha michuano mbalimbali inayosimamiwa na shirikisho la Mpira Kikapu Duniani (FIBA) na tayari wameshaonyesha mashindano mawili, Women’s AfroBasket na Men’s AfroBasket.

“StarTimes inacho kibali halali cha kuonyesha mashindano yaliyo chini ya Shirikisho la Kikapu Duniani (FIBA), hivyo udhamini huu sio bahati mbaya bali ni jitihada zetu za dhati kuhakikisha  Mpira wa kikapu unakua kwa kasi Tanzania” aliongeza Hanif.
StarTimes Super Cup imeshirikisha jumla ya timu sita kutoka jijini Dar es Salaam, timu hizo sita ni zile zilizomaliza katika nafasi sita za juu kwenye ligi ya StarTimes RBA iliyomalizika mwishoni mwa mwezi wa tisa. Timu zilizoshiriki ni pamoja na mabingwa Savio, JKT, Oilers, Vijana, Magereza na Pazi.

Aidha Hanif alitoa wito kwa mashirika na taasisi nyingi zaidi kujitoa kusaidia kukuza mchezo wa kikapu, “Jitihada za kukuza mpira wa kikapu zisiwe za StarTimes pekee, waswahili walisema “Kidole kimoja, hakivunji Chawa” hivyo ushirikiano wao ni muhimu sana katika kuhakikisha sisi sote tunafika tunapopataka”. Alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michizo Dk. Harison Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo aliahidi kushirikiana na viongozi wa mpira wa kikapu nchini.

Aliwahakikishia kuwasaidia katika kuboresha miundombinu ya mpira huo ili uweze kukua nchini.

Aidha katika fainali hiyo timu ya JKT iliibuka bingwa kwa kuichapa timu ya Oilers kwa vikapu 58 kwa 78 huku timu ya Magereza ikishika nafasi ya tatu kwa kuichapa timu ya Savio.
 
Mabingwa wa StarTimes Super Cup kwa mwaka 2017 timu ya JKT.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiwa na baadhi ya viongozi wa StarTimes na wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es Salaam.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search