Waziri Mwakyembe mgeni rasmi mkutano viongozi wa Dini...Soma habari kamili na Matukio360
Na Abraham Ntambara
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano
wa viongozi dini wenye lengo la kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kiimani, kijamii na kiuchumi.
Mkurugenzi wa Msaidizi Lugha
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Hajjat Shani Kitogo (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa viongozi wa madhehebu ya
dini uliyoandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na leo jijini Dar es
Salaam.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Hajjat
Kitogo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo
ambao utafanyika Oktoba 25/2017 .
“Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1999 Sura
ya Nane inazungumzia Malezi na inasema mafunzo ya dini yatakuwa sehemu ya
malezi ya watoto ili kusisitiza Maadili,Malezi Mema,Kazi, Kustahiana na Kuvumiliana”, alisema Hajjat
Kitogo.
Aidha amesema serikali inatambua umuhimu wa Viongozi wa Dini katika ulezi wa jamii na maendeleo ya Taifa
na ndiyo maana imeona ni vyema kukutana nao na kujadili namna gani itaweza kulisimamia taifa katika
kufikia malengo.
Naye mmoja wa washiriki wa mkutano huo Hadija Kisubi ametoa maoni yake na kusema
anaamini viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kujenga nidhamu ya kwa
taifa sababu ya neema ya mungu iliyondani ya viongozi hao pale wanatoa
maelekezo kwa umma.
Pamoja na hayo mkutano huo umebeba Kauli
Mbiu inayosema “Imani na
Uzalendo Kuelekea Uchumi wa Viwanda,” amesema.
**************************MWISHO************************
No comments:
Post a Comment