TECNO wazindua simu phantom 8 Dubai...Soma habari kamili na Matukio360..#shar
Dubai, United Arab Emirates, October 22, 2017
– TECNO, Kampuni
kubwa ya simu za mkononi TECNO iliyopo chini ya TRANSSION HOLDINGS ,
imetambulisha rasmi simu yake mpya
katika harakati zake za kukuza soko katika nchi za Asia na Africa, TECNO
Phantom 8 katika jiji la Dubai.
Matumizi ya smartphone yanakua kwa kasi
katika maeneo ya nchi za kiafrika na za mashariki ya kati kwa kiasi cha milioni
123. 7 mpaka 2016 toka milioni 106.4 mwaka 2015.
“Hivi
karibuni ripoti zinaonyesha kwa kiasi kampuni imeweza kupenya katika soko na
kuleta ushindani katika bara la Afrika
na mashariki ya kati” Alisema makamu wa rais wa kampuni mama TRANSSION HOLDINGS,
Arif
Chowdhury. “Mipango yetu ni mwaka jana ilikua kukua
zaidi kupitia mashariki ya kati hivyo kuzindua rasmi Phantom 8 jiijini Dubai ni
hatua mojawapo katika kuendeleza mipango hii. Simu zetu zitaendelea kujikita
katika kufuata mahitaji ya wateja zaidi”. Alimaliza Makamu wa raisi.
TECNO Mobile inaendelea kutoa bidhaa zenye ubora kwa wateja wake hasa
barani Africa ambapo kampuni hiyo ina nafasi kubwa katika mauzo hasa kwa nchi
kama Tanzania na Nigeria na nchi kadhaa kutokea mashariki ya kati.
Kwa zaidi ya miaka 11 TECNO imekua ikifanya
kazi ya kuunganisha wananchi katika mawasiliano kupitia simu hasa kwa kuleta
simu zenye ubora na bei inayoendana na watumiaji wake.
Simu hiyo iliyozinduliwa jijini Dubai imekua gumzo
tangu tetesi zitoke kua inakuja sokoni imezinduliwa ikiwa na jina la Phantom
8 huku ikiwa imetengenezwa kwa
teknolojia kubwa hasa kwa upande wa kamera ikiwa na megapixel 20 mbele na
kamera mbili nyuma6 GB RAM na ROM ikiwa
ni 64GB. Kwa upande wa dizaini simu inametengenezwa vizuri ikiwa na muundo wa
mithili ya Almasi na kioo.
Phantom 8
kutarajiwa kufika mabara mengine pia duniani.
Phantom 8
inauwezo wa kuweka “simcard” aina ya “Nano/ Micro” na inauwezo wa kumud memory
card ya hadi 2TB (Terra Bytes) na pia inauwezo wa 4G plus ambayo inakuwezesha
kutumia simu yako ndani na Zaidi ya nchi 200.
Kwa wateja waliopo Tanzania wataweza kuagiza simu hii mpya
katika maduka maalumu ya simu za TECNO ili kuweza kuipata inapoingia sokoni
siku chache zijazo.
Phantom 8
iliyozinduliwa hivi karibuni iikiwa imesheheni na sifa za kipekee kama Kamera,
Ubo na muonekano wa kipekee pamoja na kasi ya ajabu. Kamera ikiw ana uwezo wa
20 MP, pamoja na kamera pacha zenye uwezo wa 13Mp +12 Mp kamera za nyuma
ikiambatana na uwezo wa kuvuta picha mara 10 zaidi ya kamera ya kawaida, Ina
uwezo wa HDR,4 in 1 uwezo wa kungarisha picha,AF na mambo mengine mengi yenye
kukuhahkishia kupata picha zilizo bora na zenye muonekano mzuri.
No comments:
Post a Comment