Waziri Dk. Kalemani amsimamisha kazi Meneja uzalishaji umeme...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Salha Mohamed
WAZIRI wa Nishati, Dk. Menald Kalemani, amemwagiza Naibu
Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme-Kidatu, Mhandisi Abdalah Ikwasa
kumsimamisha kazi Meneja Uzalishaji Umeme, Manfred Ndyalu.
Hatua hiyo imefikiwa kutokana na uzembe wa Meneja huyo
kutotoa taarifa za kufyatuka kwa cable katika kituo cha uzalishaji umeme
cha Kidatu na kusababisha mitambo mingi hapa nchini kuzidiwa na umeme
kukatika.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam alipotembelea maeneo ya
uzalishaji umeme Kidatu na Ubungo Dk. Kalemani amesema serikali haiwezi
kuwavumilia watu wachache wasiojua majukumu yao.
"Hizo ni hatua za haraka ambazo tunaendela kuzichukua,
lakini tunamitambo mingi ambayo haifanyi kazi kama mtambo wa Tegeta
haufanyi kazi sawasawa na haujaanza matengenezo,”
"Lakini ni uzembe wa baadhi ya watendaji wetu, lakini
pale Kidatu mashine ya Megawat 157 bado haijaanza kufanya kazi kwahiyo
nimewaelekeza maeneo yote ambayo hazi Meneja wakuu wa uzalishaji
umeme kuhakikisha mashine zote zinzfanya kazi vinginevyo ajiuzulu
mwenyewe,"amesema.
Amesema mfumo unatakiwa kutambua tatizo linapotokea
Ubungo ambacho kimeharibika huku akimtaka Mkurugenzi wa Mfumo na
usambazaji kuhakikisha mfumo unaanza kufanya kazi la sivyo ajitafakari
kujiuzulu mwenyewe asiporekebisha.
Ameongeza kuwa serikali inahakikisha mitambo yote
iliyoharibika inakarabatiwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo ili
kupatikana umeme usiokuwa na matatizo kama hivi sasa.
Dk. Kalemani amesema kuwa serikali inafanya juhudi
kuhakikisha hadi kesho asubuhi maeneo yote ya nchi yanapata umeme huku
matengenezo ya kawaida ya kurekebisha mashine ukiendelea kama kawaida.
Amesema Shirika la Umeme (Tanesco), limewataka radhi wananchi
kutokana na matatizo yaliyojitokeza huku ikiahidi kurekebisha kasoro zilizojitokeza
ili wananchi wapate umeme wa uhakika.
No comments:
Post a Comment