TIC Yakanusha Taarifa Za Wawekezaji Kufunga Biashara Zao Nchini...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimekanusha taarifa zilizoenea kuwa wawekezaji wanafunga biashara zao huku kikibainisha kuwa taarifa hizo ni za uongo na zinafaa kupuuzwa kwani wawekezaji wanaendelea kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta mbalimabli.


Aidha, kimesema kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (tpsf) na Ubalozi wa Tanzania nchini China kimeandaa Kongamano maaluum la kuhamasisha uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na China litakalofanyika Oktoba 16 mwaka huu nchini humo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Geofrey Mwambe wakati akitoa ufafafnuzi kwa wanahabari kuhusu uvumi wa taarifa hizo.

Amesema taarifa hizo za uongo zinaenezwa na vyombo vya habari nje na kushirikiana na baadhi vya nchini visivyolitakia mema nchi huku akisisitiza hakuna mwekezaji yeyote aliyekwenda offisi kwake badala yake wanapokea mialiko mingi ya waweekezaji wanaotaka kuja kuwekeza nchini.

" Hakuna mwekezaji aliyekuja kwangu kuniambia anafunga biashara yake hizo taarifa ni uvumi unaoenezwa kutaka kupindua juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuelekea nchi ya viwanda," amaesema Mwambe.

Amebainisha kuwa wameshapokea mialiko ya wawekezaji kutoka Texas, Markani, Uturuki, Uingereza na Ujerumani na kwamba mialiko yote inaiomba TIC iende kwenye nchi hizo ikawaeleze wawekezaji hao fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Amesisitiza kuwa China hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu inaongoza kwa uwekezaji nchini iliyosajiliwa na TIC miradi 670 inayotarajia kuzalisha ajira zipatazo 83,394 yenye mtaji wa tahamani ya mtaji wa dola za Kimarekani 5,779 sawa na Sh biloni 5.8.

Aidha, amesema kati ya miradi hiyo kutoka nchi hiyo miradi 456 ni ya sekta ya viwanda sawa na asilimia 65.

Mkurugenzi huyo amaesema hata tafiti zilizofanywa na Shirika la Maendeleo ya Biashara Duniani zinaonyesha Tanzania inaongoza kuvutia wawekezaji ikizishinda nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amefafanua kuwa lengo la konagamano hilo ni kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa China zikiwemo za viwanda, kilimo, madini, mafuta, nishati, usfairishaji, miundo mbinu, ujenzi na uvuvi wa kina kirefu.

Nyingine ni usindikaji wa mazao, Afya, Teknoljia ya habari, mawasiliano na madawa.

Pia amesema konagamo hilo linatarajiwa khudhuriwa na makapuni makubwa zaidi ya 100 kutoka China na kwamba litasaidia kuitangaza nchi kama miongoni mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibaishara kwa ampuni kutoka nchi hiyo.

Mwambe amesesma ujumbe wa kituo utaondoka nchini utaongozana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akitilia mkazo wafanyabiashara wanaotaka kwenda kushiriki kongamano hilo wanakaribishwa TIC kuthibitisha ushiriki wao.

Na Hussein Ndubikile

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search