Wakati Wakielekea Kuadhimisha Siku ya Posta Duniani...TPC Wabainisha Kukabiliwa na Changamoto ya Upungufu Wa Watumaji Barua...Soma Habari Kamili na Matukio360...#share
WAKATI Shirika la Posta Tanzania (TPC) likitarajia Oktoba 9
mwaka huu kuungana na Mashirika mengine Duniani Kusherehekea siku ya posta, limesema
linakabiliwa na changamoto kubwa ya kupungua kwa kiasi kikubwa watumaji wa
barua nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
wakati wakitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa siku hiyo, Kaimu Ofisa Mtendaji
Mkuu wa TPC Deo Kwiyukwa, amesema kupukupungua huko si kwa
Tanzania pekee bali ni duniani kote.
Aidha amesema hali hiyo inatokana na maendeleo ya teknolojia
ya mtandao, alitaja moja wapo kuwa ni mjia ya email. Kutokana na mendeleo hayo
yamechangia watu kuhama katika utumaji barua wa kawaida na kutumia njia hiyo.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo Meneja Biashara-Barua
na Logistics wa TPC Jasson Kalile amesema shirika liliamua kuanzisha huduma ya
Posta Mlangoni mfumo ambao unawarahisishia kazi katika kuwahudumia wateja.
Ameeleza huduma hii mteje anapotuma barua, mlengwa wa
kupelekewa barua hiyo huipokea mlangoni mwake cha msingi ni mtumaji kuweka
anuani ya uhakika.
Amesisitiza kuwa watumaji wa barua kuhakikisha wanaandika
anuani za uhakika na pia ametoa rai kwa viongozi wa serikali za mitaa kuandika
majina na anuani za wakazi wao wanaoishi maeneo yasiyofikika kwa urahisi ili
kuwarahisishia kazi yao ya kuwafikishia barua zao.
Akigusia kuhusu mafanikio waliyopata kama Shirima Mkurugenzi huyo amesema kwamba moja ya mafanikio ni kuboresha huduma kwa umma ikiwa ni pamoja na kuweza kusafirisha baurua na vifurushi kwa haraka.
Akizungumzia shughuli zitakazofanywa siku hiyo ya maazimisho ya siku ya posta duniani, Kwiyuka amebainisha kuwa watatembelewa na wanafunzi ambao watajifunza jinsi shirika hilo linavyofanya kazi zake.
Aidha ameongeza pia watakwenda kutembelea Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo watawasaidia watoto kwa kuwachangia matibabu, hiyo
ikiwa ni sehemu yao katika kuhakikisha wanaifikia jamii.
Pia amesema siku hiyo watatoa Elimu kwa umma ili kuongeza ufahamu wao juu ya shirika hilo pamoja na jinsi ya kulitumia kwa ajili ya maendeleo.
Pia amesema siku hiyo watatoa Elimu kwa umma ili kuongeza ufahamu wao juu ya shirika hilo pamoja na jinsi ya kulitumia kwa ajili ya maendeleo.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment