Wanasiasa washauriwa kuiga mfano viongozi wa dini..Soma habari kamili na Matukio360
Na Hussein Ndubikile
VIONGOZI wa Kisiasa nchini wameshauriwa kuwa wepesi kujenga utamaduni wa kuiga mfano wa viongozi wa dini panapotokea tofauti kwa kutumia njia ya majadiliano ili kupata maridhiano yatakayoendelea kuimarisha na kudumisha umoja na amani ya nchi.
VIONGOZI wa Kisiasa nchini wameshauriwa kuwa wepesi kujenga utamaduni wa kuiga mfano wa viongozi wa dini panapotokea tofauti kwa kutumia njia ya majadiliano ili kupata maridhiano yatakayoendelea kuimarisha na kudumisha umoja na amani ya nchi.
Waziri mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
Pia wameonywa kuacha kutumia vyombo vya habari kuelezea
tofauti zao kwani kufanya kunaweza kuwagawa wananchi na kuhatarisha amani
iliyopo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dr es Salaam na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni Jaji Mstaafu, Joseph
Warioba katika Mdahalo wa Mashauriano Juu ya Umuhimu wa Kuhimiza, Kulinda na
Kudumisha Amani na Umoja nchini ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Amesema viongozi wa dini wamekuwa wepesi kukutana kujadili
masuala yanayohusu amani ya nchi huku akibainisha suala hilo ni tofauti kwa
wanasiasa kwani huvitumia vyombo vya habari kulumbana hata wakati mwinginge
kuwagawa wananchi hali inayohatarisha ustawi wa amani.
" Viongozi wa dina wanatusaidia sana kuimarisha umoja na
amani makanisani na misikitini nawaomba wanasiasa muige mfano huu na sio
kutumia vyombo vya habari tuache malumbano yasiyo na msingi kwani nchi nyingi
zimepata matatizo sababu ya kushindwa kutumia mtindo wa maridhiano, "
amesema.
Amebainisha kuwa viongozi wa dini na siasa wana ushawishi
mkubwa kwa wananchi hasa pale wanapotumia maneno yanayoweza kujenga au kubomoa
amani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James
Mbatia amesema viongozi hao wanatakiwa kutambua mchango wao katika hivyo
waendeleze ushirikano kwa masilahi ya taifa.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Nurdin Mangochi ameiomba
Serikali kuwasaidia usafiri wa pikpiki, magari na baiskeli ili waweze kuyafikia
maeneo yasiyoweza kufikikika kiurahisi na kwamba itasaidia kufundisha
mafuundisho mema yenye kuhimiza amani, umoja na upendo.
Amewaasa wanasiasa kufuata misingi ya kuishi kibinadamu
ikiwemo ya kuhheshimu rasilamali watu, mamlaka, ardhi pamoja kukubali matokeo
yanapotangazwa kuepuka machafuko.
Amefafanua kuwa kinachosababisha wanasiasa kutofautiana ni
kutokana na kuwa na mitazamo taofaui ya kivyama huku akisisitiza viongozi wa
dini wanahubiri jambo moja ambalo ni umoja na amani.

No comments:
Post a Comment